ALIKIBA AMBURUZA VIBAYA DIAMOND

Mon media
0




Na Amon Laurian

Alikiba Amgaragaza Vibaya Diamond Platnumz


Jukwaa la kidijitali la kupakua na kusikiliza muziki la Boomplay limetoa orodha rasmi ya wasanii wa Bongo Flava ambao walisikilizwa zaidi ndani ya wiki moja iliyopita.




Licha ya msanii Diamond Platnumz kutoa nyimbo zaidi ya tatu katika kipindi cha wiki tatu zilizopita, wengi wameshangaa kutomuona msanii huyo kwenye orodha hiyo ya wasanii sita.




Orodha hiyo inaongozwa na msanii Alikiba ambaye amezidi kutamba na wimbo wake wa Sumu aliomshirikisha Marioo, wenye mtindo wa Amapiano.




Katika nafasi ya pili, Mbosso ametaradadi akifuatwa na Juma Jux ambaye nafasi yake imehakikishwa na mapokezi mazuri ya wimbo wake wa Enjoy alioshirikisha Diamond Platnumz.




Harmonize anafunga nne bora huku nafasi za tano na sita zikishikwa na malikia wa Bongo Fleva Zuchu na Nandy mtawalia.




“Tunavyomaliza wiki nyingine, hawa ndio wasanii pamoja na albamu zilizofanya vizuri. Unayempenda yupo? Endelea kustream nyimbo zake aweze kubaki au kuingia kwenye chart hii.




"Chati hii inatokana na idadi ya streams kuanzia tarehe 14 Julai mpaka tarehe 20 Julai mwaka 2023. Streams za Boomplay zinahesabika kwenye chati za Billboard,” Boomplay walisema.




Katika albamu zilizoshika kasi katika wiki hii, Harmonize alifana na albamu yake ya Made For Us akifuatwa na abamu ya Mbosso, Khan na Love Sounds Different yake Barbana, bwana harusi mpya mjini.




Rayvanny alishika nafasi ya nne na albamu yake ya Flowers III nafasi ya nne ikichukuliwa na msanii pekee kutoka Nigeria, Omah Ley.


-------------------

Tags

Post a Comment

0Comments
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top