MSANII WA MAREKANI P DIDY AVAMIWA NA MAOFISA WA USALAMA

Mon media
0


 Nyumba za mwanamuziki wa HipHop wa Marekani Sean Love Combs almaarufu Puff Daddy au P. Diddy zilizopo Los Angeles na Miami zimevamiwa na Idara ya Usalama wa Taifa kwa uchunguzi wa madai ya kesi zinazomkabili za unyanyasaji wa kijinsia na biashara ya ngono.


Watu hao wa Usalama wa Taifa Marekani waliwapiga pingu watu watatu waliowakuta nyumbani kwa Diddy wawili kati yao wakiwa ni watoto wake Christian Combs na Justin Combs. 


Baada ya taarifa hizo Diddy alionekana uwanja wa Ndege wa Miami, na ndege yake binafsi kufuatiliwa mpaka visiwa vya Caribbean.


Tags

Post a Comment

0Comments
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top