WOLPER AWEKA WAZI NDOA YAKE KUWA HATIANI

Mon media
0


 Jackline Wolper amekiri kwamba kwa miezi tisa sasa ndoa yake imekuwa ikipumulia mipira Kwasababu yeye na mume wake hawako sawa tangu mwezi wa sita mwaka jana. Amesema kwa sasa wanalea watoto tu lakini suala la wao kuwa karibu kimahusiano limekuwa likileta mgongano kila kukicha.


Pia Wolper ametengua kauli yake aliyowahi kuisema mwaka jana kuwa hata akimkuta mume wake anachiti na mwanamke mwingine atamuacha au atamvisha nguo kabisa na kumrudisha nyumbani Kwasababu pesa ambayo mume wake anaipata kwa huyo mchepuko inasaidia familia.


Amesema anafuta kauli hiyo Kwasababu aliiongea akiwa amelewa chakali, amesema akimfumania mume wake ndio utakuwa mwisho wa mapenzi yao. Rich ambaye amezaa na Wolper amekuwa na matukio vululu_vululu ya kuhusishwa kutoka kimapenzi na wanawake mbalimbali wa mjini licha ya kuwa na sura ya upole mfano wa kondoo anayekiribia kuchinjwa.

Tags

Post a Comment

0Comments
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top