ISHU YA KIBU KUGOMA KUONGEZA MKATABA SIMBA IKO HIVI

Mon media
0

 



Wakati sakata la kiungo mshambuliaji Kibu Denis kugoma kusaini mkataba mpya Simba SC likiendelea kuchukua nafasi kubwa katika mitandao ya kijamii, Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Ahmed Ally ameibuka na kudai kuwa bado wana kikosi bora na imara.


Suala la Kibu Denis kugoma kusaini Mkataba mpya klabuni hapo huku ule wa sasa ukibakisha mwaka mmoja, liliibuliwa jana Alhamis (Aprili 02), ikidaiwa amekuwa akiupiga chenga uongozi wa klabu hiyo na tayari Azam FC na Young Africans zinatajwa kumuwania Mshambuliaji huyo.


Ahmed Ally ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwaaminisha mashabiki na wanachama wa Simba SC kuhusu kikosi chao, akisisitiza kuwa pamoja na kupata matokeo mabaya msimu huu bado klabu hiyo inaongoza kwa wachezaji wake wengi kuhusishwa na klabu za ndani na nje ya Tanzania katika kipindi hiki cha kuelekea mwishoni mwa msimu.


Ahmed Ally ameandika: SIMBA INA KIKOSI BORA SANA.

Licha ya timu yetu kusemekana ni mbovu lakini ndio timu inayoongoza kwa wachezaji wake kuhitajika na vilabu vingi zaidi vya ndani na nje nchi


Ni dhahiri kuwa tuna kikosi chenye wachezaji bora


Hatujapata matokeo mazuri msimu huu lakini haindoi ukweli kuwa wachezaji wetu ni bora sana ndio maana wanatajwa sana sokoni


Tunachoenda kukifanya hivi sasa ni kubaki na wale bora wenye moyo wa kuitumikia Simba


Katika dirisha hili la usajili tunaemtaka atabaki Simba lengo ni kutengeneza Simba tishio turudi kwenye Ufalme wetu.

Tags

Post a Comment

0Comments
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top