MBAPPE AANDALIWA JEZI HII MADRID

Mon media
0


 Mshambuliaji wa Paris Saint German (PSG), Kylian Mbappé amethibitisha ataondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu kujiunga na Real Madrid iliyomuandalia jezi namba 9. 


Ndani ya kikosi hicho cha Madrid, Mbappé atavaa jezi namba 9 iliyokuwa inavaliwa na Mfaransa mwenzake Karim Benzema.


Video ya Mbappe kupitia picha jongeo kwenye mitandao ya kijamii ingawa hajabainisha ni wapi ataelekea, lakini Madrid inatajwa anakwenda Madrid alikoandaliwa jezi namba hiyo. 


PSG hawajamjumuisha Mbappe kwenye chapisho la kutangaza jezi zao mpya hali inayoashiria kuwa nyota huyo raia wa Ufaransa hayupo kwenye mipango yao ya msimu ujao.


Inaaminika kuwa mfungaji huyo wa muda wote wa PSG tayari amefikia makubaliano ya kujiunga na vigogo wa Uhispania, Real Madrid ingawa hakuna klabu iliyoweka bayana ukweli huo.


Baadhi ya wachezaji wa PSG wameonekana kwenye chapisho la klabu hiyo kwenye mitandao ya kijamii wakiwa na jezi hizo mpya, wakiwemo Marquinhos, Nuno Mendes na Lucas Hernandez lakini Mbappe hakuonekana.


Tags

Post a Comment

0Comments
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top