JINSI NANDY ALIVYOWAFUNGULIA NJIA MASTAA KIBAO

Mon media
0


 Msanii wa Kike nchini kwenye miondoko ya Bongo Flava, Nandy a.k.a The African Princess aliufungua vizuri mwaka 2024 baada ya mwezi Januari kuachia Hit inayoitwa DAH ambayo ilifanya vizuri na kuzalisha remix kadhaa ikiwemo na Alikiba ambayo ilifanya vizuri zaidi.


Ukubwa wa Remix hiyo, ulimfikia Mwanamuziki wa RnB nchini Marekani, Usher Raymond ambaye alim-DM Nandy akiomba beat ya wimbo huo ili aingize verse.


Ilikuwa ni Big story kwenye social media ambayo iligawa watu kwenye mitazamo tofauti, na hii ni baada ya Nandy mwenyewe kuuonyeshea Umma chats zake na Usher Raymond kwenye Insta Story yake.


Wapo waliotamani Nandy angesubiri kwanza ngoma itoke ndio aweke chats na Usher, hawa pia waliona kilichofanyika ni Ushamba, wengine wakidai watu wataroga na ngoma haitafanyika.


Baadhi ni wapambe wa mastaa wakubwa wakasema, Usher hana maajabu kimuziki kwa sasa, hivyo jambo hilo kulifanya kubwa ni ushamba tu. Baadhi waliona Nandy yupo sawa na ni hatua kubwa kwake kimuziki.


Baada ya miezi kupita, kwasasa imekuwa trend wasanii kuweka hadharani chats zao na mastaa wa nje, ilianza kwa Harmonize na Meek Mill, ikaja kwa Diamond Platnumz na Jason Derulo, Roma Mkatoliki na Jadakiss, na Fid Q akiwa kwenye kolabo ambazo kuna Jadakiss na The Game ndani.


Kifupi ni kuwa, kile kilichoitwa ushamba kwa Nandy, ndicho kilichogeuka Ujanja ume kwa wasanii wengine🙌

Tags

Post a Comment

0Comments
Post a Comment (0)

#buttons=(Accept !) #days=(20)

Our website uses cookies to enhance your experience. Learn More
Accept !
To Top